ZITTO KABWE ATOLEA UFAFANUZI KUHUSIANA NA TUHUMA ZINAZOMKABILI

darmpya#darmpya: Jeshi la Polisi nchini, limekuwa likituhoji kwa tuhuma mbili.
1) Kutumia takwimu halali kupotosha umma kinyume na kifungu cha 37 cha sheria ya takwimu ya Mwaka 2015 na
2) Kutumia mitandao ya kijamii kusambaza habari za upotoshaji kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015.

Nilikubali tuhuma namba (1) kwamba nyaraka walizonazo za uchambuzi wa takwimu za ukuaji wa Pato la Taifa ni za chama chetu cha Act Wazalendo na
(2) Kwamba nilitumia mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter na WhatsApp kusambaza uchambuzi huo wa takwimu.
Polisi hawaridhiki, wamechukua simu yangu ili kuthibitisha kama nasema kweli kuwa nyaraka zile ni zetu na nilisambaza. Wamevamia ofisi ya chama kutaka kuchukua kompyuta iliyochapa uchambuzi ule. Mimi nimekiri lakini bado eti hawaamini. Hawaamini kuwa nimekiri. Hawa sio polisi, ni vichekesho.

Hizi ni mbinu za kutuharasi. Ni mbinu za kutafuta chanzo cha habari zetu kwani waliponihoji walitaka kujua Mimi nilijuaje kuwa takwimu zimepikwa. Ni mbinu za kutaka chama kisishiriki kikamilifu kwenye kampeni za udiwani kwenye kata 43 na kuwaeleza wananchi namna Serikali ya Awamu ya Tano inavyominya Haki za Raia na kuangusha uchumi wetu.

Nimewaambia polisi kuwa wanipeleke mahakamani. Waache usumbufu huu, twende mahakamani. Kesi hii ya kwanza kuhusu sheria ya takwimu ndio itakuwa ya mwisho kwani tumejipanga vya kutosha 1) kuonyesha umma kuwa uchumi wetu umesinyaa tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani na 2) sheria ya takwimu haizuii uchambuzi wa takwimu kutoka mamlaka halali.
Serikali hii ya Awamu ya Tano inaongoza kwa ulaghai ( manipulation) kuliko Serikali zote zilizowahi kupita katika nchi yetu. Manipulation is never sustainable.
Kwa wanachama wa ACT Wazalendo na wana demokrasia wote naomba muwe watulivu na mkumbuke maneno haya “ kwanza wanakudharau, kisha wanakucheka, kisha wanapambana na wewe kisha unashinda “. Tutawashinda

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*