Zitto Aachiwa, Polisi wachukua simu yake, Ofisi za ACT Wazalendo kupekuliwa kutafuta nyaraka za kusinyaa kwa Uchumi

darmpya#Updates: Zitto Aachiwa, Polisi Wachukua Simu yake, Ofisi za ACT Wazalendo kupekuliwa kutafuta nyaraka za kusinyaa kwa Uchumi

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Kabwe Ruyagwa Zitto, leo aliripoti Kituo cha Polisi Kamata Jijini Dar es Salaam kama alivyoamriwa awali na Jeshi hilo.

Inadaiwa kuwa, baada ya kiongozi huyo kutii amri ya Jeshi la Polisi, askari walichukua simu yake kwa maelezo kuwa itasaidia uchunguzi wao, na wameahidi kuwa watairudisha kwake kesho jioni, na ametakiwa kurudi kituoni hapo Novemba 21, 2017.

Pia Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa litakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo, kwa Lengo la kufanya upekuzi wa Ofisi hizo wakitafuta nyaraka zilizotumika na Chama kufanya Uchambuzi wa Takwimu za Serikali ambao unaonyesha Uchumi wa Nchi yetu “UNASINYAA”.

Ado Shaibu
Katibu – Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma
ACT Wazalendo
Novemba 7, 2017
Dar es salaam

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*