ZIARA YA NDG POLEPOLE UVCCM TAIFA:WASIYO WAADILIFU HAWATAPEWA DHAMANA ZA UONGOZI

Katibu wa (NEC) Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole Leo 6 June,2017 amefànya Ziara na Kikao cha ndani katika Ofisi ya Umoja wa VIJANA MAKAO MAKUU YA Jumuia hiyo na kukutana na Uongozi wa UVCCM Taifa.Wakiongozwa na Kaimu Kaimu Katibu mkuu wa Jumuia ya Umoja wa Vijana Ndugu Shaka Hamdu Shaka pamoja na Wakuu Wote sita wa Idara ndani ya Jumuiya Hiyo.

Wengine Waliyokuwepo ni Makatibu pamoja na Wenyeviti wote wa Wilaya na Mkoa wa Dar ES Salaam.Pamoja na Secretariet ya UVCCM Taifa.

Ndugu Humphrey Polepole ameonya Suala la baadhi ya Viongozi ndani ya Jumuia kuhusika na kupanga Safu na Kutengeneza Mtandao wa Watu wasiyo Waadilifu na wa Hovyo katika Chama Chetu.

Akizungumzia kuhusu Maadili Ndugu Polepole amesisitiza kwa Mkuu wa Idara ya Usalama na Maadili kuhakikisha wanamshauri Ndugu Shaka na kumsaidia kupata Wagombea Waadilifu,Wachapakazi, Wawajibikaji na Wasiotoa Wala kupokea Rushwa.

Ndugu Polepole amewasisitiza Umoja wa Vijana wasijaribu wala kuthubutu kuwapitisha Wagombea wasiyo kuwa na Sifa ndani ya Chama na amewambia yeyote atakayehusika kupanga na Kuwabeba Wagombea wenye nia ya Kupanga safu ndani ya CCM MPYA na TANZANIA MPYA.Hatobaki salama Mtu na Wote Watashughulikiwa na Vikao husika vya Maamuzi Mara Moja.

Akizungumzia Kuhusu Utendaji haki katika shughuli za Jumuia za Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi. Ndg Polepole amesisitiza tena asili ya Chama Cha Mapinduzi ni vitu viwili,Haki na Watu kama ambavyo imeelezwa katika Kitabu Cha CCM na Raia. Akaendelea kuweka msisitizo kwamba jumuia ya Umoja wa Vijana lazima iwe kioo cha kuonesha Uhalisia huo Kwa Matendo, Kwa Maneno na fikra zake.

Amewaambia kuwa Chama Cha Mapinduzi nchini na Barani Afrika kwa Ujumla ndiyo Chama Pekee kinachojulikana kwa kutenda Haki na Duniani kote inajulikana hivyo hivyo.

Ndg Polepole aliongeza kuwa Uongozi wa Chama unaamini haki itatendeka katika Mchakato huu na Amemwambia Kaimu Katibu Mkuu Shaka kuendeleea kutenda haki kama anavyowajibika kwa sasa.

Akizungumzia pia kuhusu swala la Uchumi.Ndugu Polepole Maslahi ya Watumishi amesisitiza Mkuu wa Idara ya Fedha UVCCM Taifa kuhakikisha watumishi wote wanashughulikiwa Maslahi Yao bila upendeleo na kuweka Mpango kazi wenye kuonesha dira ya Jumuia ili kuinua Uchumi wa Jumuiya na Wafanyakazi.

Naye kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM TAIFA Ndg Shaka Hamdu Shaka Amesema kufikia Mwezi Septemba 2017 Watakuwa Wamelipa madeni yote na Malimbikizo ya Madeni.

Ndugu Polepole, Amesisitiza Umoja, Mshikamo Lakini kipekee alisisitiza kukosoana kwa nidhamu hasa kwa Vikao vya Ndani na Viongozi wakubali kukosolewa na wakubali Kujirekebisha kwa Maslahi ya Chama na Nchi Yetu Tanzania.

AHSANTEN SANA.