WIZKID AWAKERA MASHAKIBI WAKE LONDON

Wakati Staa kutoka Nigeria Wizkid Ayo, akitengeneza rekodi kubwa ya kuwa msanii wa Kwanza Barani Afrika kujaza mashabiki katika ukumbi wa Royal Albert Hall huko jijini London, Unaambiwa kwamba jamaa Alichelewa kuingia stejini kwa muda usiopungua masaa mawili.

Ishu hiyo imepelekea baadhi ya mashabiki kumshangaa Wizkid katika siku yake ya Kihistoria kama hiyo na kushindwa kufanya show kwa wakati.

Nikuchane tu mwana Darmpya ni kwamba Ukumbi wa Royal Albert Hall unabeba jumla ya watu 5,544 na wakati anamaliza show yake hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo alisema kwamba hatua yake nyingine ni kuijaza O2 Arena.