WAZIRI NCHEMBA AWATAKA WATANZANIA KUTOCHANGANYA UTAWALA WA SHERIA NA UDIKTETA.

Na John Marwa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh.Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kutochanganya utawala wa sheria na Udikteta.

Waziri Nchemba aliyasema hayo leo jioni katika mkutano na wananchi wa Kimara Jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, alisema Watanzania walio wengi bado hawafahamu nini maana ya utawala wa sheria na kwamba Rais Magufuli ni mfuata sheria sio Dikteta kama baadhi wanavyodai.

Alisema, Rais anatutengenezea uchumi wa kujitegemea,tulikuwa tunapigwa Kwenye madini na sekta zote,sasa hatua zinachukuliwa.

“Hii nchi ingekuwa na udikteta hao wapinzani wasingekuwa wanashiriki uchaguzi,kwenye udikteta hakuna uchaguzi wala Bunge, Rais Magufuli anazuia wanyonge kuonewa,huu si udikteta,” alisema Mh.Nchemba.

Alisema, zamani hela ndo ilikuwa inaamua nani apate haki,hela ingeweza kukutoa hata chumbani kwa mke wako.

Aidha alibainisha kuwa, ukimchagua mgombea wa CCM atatekeleza ahadi zake kwa sababu atarudi tena 2020, mkimpa mpinzani hatafanya kitu ili c ionekane haijafanya kitu.

“Rais lazima awe mkali kwa sababu hata makanisani shetani anakemewa kwa ukali,uovu huondolewa kwa ukali, Mbowe anataka rais awachekee wezi wa almasi,na mafisadi, rais anasimamia sheria na sio,” akasema.

Ilani,sera na serikali iliyo madarakani ni ya ccm,hivyo wananchi naomba mchague ccm ili iendelee kutimiza ahadi zake Rais Magufuli ameanzisha mahakama ya mafisadi ili ikatende haki,angekuwa dikteta angewanyonga mafisadi bila kuwapeleka mahakamani, alisisitiza Mh. Nchemba.

Waziri Nchemba alisema, atawashangaa wananchi wasipoichagua CCM wakati ilani inayotekelezwa nchi hii ni ya CCM na kwamba kule Mwanza Rais alisimamisha kuwafukuza machinga kwa sababu mbunge alipeleka maombi kwa Rais,wapinzani wao ni kelele tu.

Kuwaombea Matajiri washushwe wawe masikini ni mawazo ya kijinga,mwenzako akitatuliwa shida nawe peleka zako.

“Wanalia demokrasia wakati toka enzi za Mkapa mpaka leo wao wanaongoza chama chao kama Kampuni.

Akizungumzia bomoa bomoa zinazoendelea Mkoani Mwanza, Mh. Nchemba alisema, Rais hajapendelea kuhusu bomoa bomoa,amesikiliza kilio cha wananchi wake akasimamisha bomoabomoa kule Mwanza.

Sanjari na hilo, Waziri kama Waziri wa usalama, alipiga marufuku kumzomea mwanachama wa chama kingine kisa tu amevaa sare ya chama chake:Mwigulu Kimara.

Kwa upande wa bomoa bomoa ya Kimara alisema, wamebomoa pake Kimara ili kuboresha Jiji la Dar es Salaam na kwamba huwezi kulinganisha Jiji hili na Mwanza.

Rais amejenga barabara kubwa Arusha na Moshi,kama angekuwa anabagua ambao hawakumchagua asingefanya hayo, mkiwachagua Wapinzani nitazuia mkutano wao wa kuja kuwapongeza kwa sababu watakuja kutukana hapa.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*