WATU 26 WAMEUAWA NA WENGINE 20 KUJERUHIWA NA RISASI HUKO TEXAS MAREKANI.

Kanisa la Sutherland Springs lililoshambuliwa kwa risasi na kusababisha watu zaidi ya 26 kuuawa na zaidi ya 20 kujeruhiwa. Kanisa hili lipo umbali wa kilomita 40 Kusini Mashariki mwa San Antonio mjini Texas nchini Marekani.

Watu zaidi ya 26 wanadaiwa kuuawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa kwa risasi hapo jana katika kanisa la mji mdogo wa vijijini Texas Marekani.

Watu hao waliuawa angalau 26 waliuawa baada ya mtu mmoja kufyatua risasi wakati ibada ya Jumapili ikiwa inaendelea katika la  kanisa la Sutherland Springs lililoko katika mji mdogo uliopo vijijini kwenye mji wa Texas.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Msemaji wa Idara ya Usalama wa Umma mjini Texas, Sheriff Wilson County Joe Tackitt alisema, haya ni mauaji makubwa kutokea nchini humo.

Kanisa la Sutherland Springs, lipo umbali wa kilomita 40 Kusini Mashariki mwa San Antonio mjini Texas.

Alisema kuwa, waathirika waathirika wakubwa katika tukio hilo ni wa umri wa  miaka mitano hadi 72.

Mamlaka za usalama nchini humo zinaendelea na uchunguzi zaidi wa tykio hilo ambapo mtuhumiwa wa tukio hilo alipatikana akiwa amekufa katika gari lake karibu na makutano ya FM 539 na Sandy Elm Road katika kata ya Guadalupe, Texas.

“Mshtakiwa huyo, mwenye umri wa miaka 26, pia amekufa baada ya kufanya mauaji hayo huko huko katika Kanisa la Kwanza la Baptist,” alisema msemaji wa mamlaka hiyo.

Mashambulizi yalianza saa 11:20 asubuhi baada ya mtuhumiwa kuonekana kwenye kituo cha gesi cha Valero huko Sutherland Springs, akivaa kofia nyeusi kufunika sura.

Idara ya Usalama wa Umma ilisema,  mtuhumiwa huyo alitoka ndani ya gari lake alivuka barabara kwenda katika kanisa huku akikimbia.

Mtuhumiwa alianza kufyatua risasi upande wa kulia wa kanisa na akaendelea kufyatua risasi nyingi kisha akatupa silaha na kuanza kukimbia.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*