WASICHANA SABA WAKAMATWA   BAADA YA KUJIFANYA WAISLAMU HUKO NIGERIA.

Wasichana saba waliojifanya kuwa Waislamu kwa kuvaa vazi la hijab wamekamatwa nchini Nigeria kwa kujaribu kufanya safari haramu ya barani Ulaya ,kulingana na maafisa.

Wasichana hao ni miongoni mwa watu 12 waliokamatwa na maafisa wauhamiaji mapema wiki hii walipojaribukuvuka mpaka kaskazini mwa jimbo la Katsina wakielekea Ulaya.

Mamlaka ya uhamiaji inasema kuwa wasichana hao saba wanatoka Kusini mwa taifa la Nigeria, na walivalia vazi la Kiislamu ili kuwasaidia kupita kwa urahisi katika mpaka katika eneo la kaskazini lililo na Waislamu wengi.

Baadhi ya waliokamatwa walinukuliwa wakisema kwamba walitaka kwenda Ulaya ili kutafuta ajira kutokana na hali ngumu ya maisha nchini Nigeria.

Wasichana hao baadaye walikabidhiwa kwa kitengo cha kukabiliana ulanguzi wa watu kwa uchunguzi zaidi.

Takriban watu 40 wamekamatwa katika kipindi cha miezi minne iliopita nchini Nigeria wakijaribu kuvuka na kuingia nchini Niger ili kuelekea Libya kupitia jangwa la sahara kabla ya kuabiri boti na kuelekea Ulaya.

Wakati huohuo zaidi ya watu 1000 waliripotiwa kurudi wenyewe nchini Nigeria kutoka Libya katika kipindi chamiezi mitano.

Source BBC.