WASANII WA BONGOFLAVA WANATENGENEZA KIKI BADALA YA MZIKI MZURI:NAY WA MITEGO

Msanii Nay wa Mitego amefunguka na kusema kuwa ndani ya miaka miwili au mitatu inayokuja anaona wazi muziki wa bongo fleva unakwenda kufa kama ambavyo tasnia ya filamu bongo ilivyokufa kwakile anachodai wasanii wamekuwa wazembe na kutegemea kiki.

Nay wa Mitego amesema kuwa wasanii wengi wa bongo saizi wanategemea zaidi kiki kuliko kufanya muziki mzuri jambo ambalo anaona litafanya muziki wa bongo kufa muda si mrefu kama wasanii hao hawatachukua jukumu la kurudisha muziki kwenye mstari.

“Kusema kweli kuna kitu nakiona kwenye muziki wetu wa bongo fleva tunakibarua kikubwa cha kurudisha muziki kwenye mstari sababu saizi watu wanatengeneza kiki kubwa ila muziki mdogo, yaani kiki zimekuwa mbele muziki unasindikiza kiki miaka miwili mitatu ijayo naiona bongo fleva ikiwa imepotea kama bongo movie ambavyo imepotea kama tusipokuwa makini kuamua kufanya kazi kweli na kiki ziwe tu kusindikiza muziki, saizi watu wanatengeneza kiki hata hazielezeki wasanii tunajisahau tuamke, turudishe muzikiwetu kwa sababu tunawalemaza hata mashabiki” alisema Nay wa Mitego

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*