VURUGU ZAIBUKA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA KENYA

Vurugu zimeibuka katika kituo cha kupigia kura cha Kariokor Social Hall Jijini Nairobi ambapo polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kutuliza hali ya mambo.

Vurugu hizo zilisababishwa na wapiga kura waliokua wanalazimisha kuingia katika  kituo cha kupigia kura bila ya kufuata utaratibu. Wananchi  wamewalaumu maafisa wa tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC kwa maandalizi duni yaliyosababisha msongamano wa watu  wengi hali iliyopelekea kuzuka kwa vurugu hizo kwani wananchi walikua wanawania kuwahi kuingia ndani ya kituo cha kupigia kura.

Katika vurugu hizo mwanamke mmoja amevunjika mguu na mwingine akipata majeraha madogo madogo .

Majeruhi  wote hao wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.