VITA YA MANENO YAZUKA TENA BAINA YA TRUMP NA RAIS WA KOREA KASKAZINI.

Haki miliki ya picha EPA Image caption Vita  ya maneno yazuka tena Baina ya Trump na Rais wa Korea Kaskazini

Rais wa Marekani na Korea Kaskazini wamerejelea vita yao ya maneno kufuatia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Korea Kaskazini ilimuita Trump kuwa “mchochezi wa vita na mzee” na kusisitiza kuwa haiwezi kamwe kuachana na mipango yake ya nyuklia.

Rais Trump alijibu kwa kuandika katika mtandao wake wa kijamii wa Tweeter kuwa, anashangaa ni kwa namna gani Kiongozi wa Korea Kaskazini anamuita mzee.

Aidha Trump alieleza kuwa Ni kitu kimoja tu kitafanya kazi dhidi ya Korea Kaskazini na kuongeza kwamba Hakuna uwezekano wa kutokea vita vya nyuklia na Korea Kaskazini.

Kwa maneno yake, Bwana Trump alisema kuwa hatamuita Rais Kim Jong-un, kuwa mtu “mfupi na mnene”. pia katika hali ya kushangaza  Trump ameibuka nakusema kuwa anajaribu sana kwamba siku moja atakuwa rafiki wake wa karibu ambaye watashirikiana katika maswala mbali mbali ya kiutawala kwa manufaa ya mataifa yao mawili.

Trump awali alimkejeli kiongozi huyo mkuu wa Korea Kaskazini, kwa kumuita mwendawazimu na ‘mtu wa kuunda zana za roketi’. Ni mda wa miezi kadhaa sasa viongozi hao wawili wamekua katka mchuano mkali wa maneno chanzo ikiwa ni mpango wa siraha za nyukilia unao pangwa na korea ya kasikazini.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*