UVCCM WAZINDUA SEMINA YA UJASILIAMALI DAR ES SALAAM.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo ameshiriki na kuzindua semina elekezi ya ujasiriamali kwa vijana wa wilaya ya Ubungo ili kushiriki kwa ukamilifu maonesho saba saba hayo yanayoanza terehe 1 Julai 2017.

Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Texas Manzese jijini Dar es Salaam

Malengo ya semina hiyo ni :

Kukusaidia mjasiriamali na mfanyabiashara vijana kuweza kutanua soko lao la kibiashara.

Kufungua Fursa mbalimbali za kiuchumi kwa vijana ambapo wamepata fursa ya kukutana na makundi mbalimbali ya wajasiriamali wadogo na wakubwa. n.k

Kusaidia vijana namna ya kuunda vikundi na hatua zake ili vitambulike kisheria.

Katika semina hiyo wamealikwa wataalamu mbalimbali ambao watatoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kuziona FURSA na namna ya kuzitumia.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake aliwemo Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya kinondoni Said Masanga.