UNCTN MOROGORO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUTOA MSAADA

Na Jyross Curtis

Taasisi ya umoja wa mataifa kwa vijana walioko sekondari ya UNCTN mkoa wa morogoro kwa ushirikiano na wadau mbalimbali imeweza kuadhimisha siku YA mtoto wa Afrika kwa ukanda wake kwa kutoa msaada wa vitu vidogo vidogo kwa watoto yatima wanaopatikana katika kituo cha Mgolole.

Siku ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila tarehe 16 June ikiwa ni azimio la nchi wanachama wa umoja wa Afrika waliazimia azimio hilo ikiwa kama ishara ya kukumbuka mauaji ya kikatili yaliyowahi kutokea kwa watoto huku nchini Afrika Kusini, tukio hilo lilifuatia baada ya watoto wa shule ya msingi (watoto wa Kiafrika) kudai haki yao ya kutokubaguliwa.

Umoja wa nchi za kiafrika (AU) ulipitisha azimio hilo kwa kwa ushirikiano na jumuiya ya umoja wa mataifa (UN) mnamo mwaka 1990.

Aidha katika maadhimisho yaliyofanywa na vijana wa asasi ya umoja wa mataifa mkoa wa morogoro yamekuwa kielelezo stahiki kumuonesha na kumueleza mtoto kuwa ni mchango mkubwa wa maendeleo ya taifa “Yatupasa kuwalinda na kuwajali watoto wetu kwa hali zote kwani hawa ni asset kubwa ya mafanikio ya baadae ya taifa na Afrika kwa ujumla wake” alieleza Mwenyekiti wa UNCTN mkoa wa morogoro Ndg. Abdallah Njayagha.

Pia wakiwa katika kongamano la maadhimisho hayo, Katibu msaidizi wa UNCTN mkoa wa Morogoro nae hakukaa kimya hivyo alinyenyua sauti yake juu ya watoto na kusema kuwa “Mtoto wa Afrika ni mtoto mwenye akili kubwa mno lakini mtoto huyo anapitia vikwazo na changamoto nyingi katika maisha ndani ya jamii yake” akaongeza kuwa “Jamii zimejisahau kumpa mtoto wa Afrika matunzo stahiki akiwa katika kipindi kidogo na hivyo kupelekea kuharibika na kuharibu ndoto zake za baadae.” Alisema Ndg. Katibu msaidizi.

Awali vijana hao wa UNCTN mkoa wa morogoro walijitoa kwa kusaidia baadhi ya kazi ndogo ndogo katika kituo cha watoto yatima cha Mgolole kwa kufyeka majani, kufanya usafi na kucheza michezo mbalimbali na watoto kama sehemu ya kuwafariji ili wajisikie kuwa hawako wapweke.

Sister wa kituo cha watoto yatima wa Mgolole alisita kukaa kimya kueleza furaha yake juu ya uwepo wa vijana hao, Akiongea na mwandishi mashuhuli wa Darmpya.com, Jyross Curtis, alisema kuwa anayo furaha kuona kuwa watu wanawaona na kuwawaza “Nafurahi kuona kumbe watu wanatuona na wanatuwaza hadi kufikia hatua ya kutuunga mkono kwa jambo kubwa na dogo pia. Nafurahi kuona vijana wadogo ambao bado wako shuleni wanasoma kutuletea msaada mkubwa kama huu, wameleta nguo, viatu, na vinginevyo, ni nguvu ya kujitolea imewasukuma” alieleza, pia aliongezea kwa kuwaomba wanajamii kuwakumbuka zaidi “Watoto wanahitaji msaada na pia wanahitaji nguvu kubwa zaidi ili waweze kukua vyema, msaada wa wanajamii utatusaidia katika kuwajenga watoto wetu” alimaliza.

Halikadharika vijana wa UNCTN mkoani Morogoro waliieleza Darmpya.com kuwa watoto ndio ngazi kubwa ya kwanza ya maendeleo ya taifa lolote na hivyo wanastahili msingi mzuri wa malezi na wenye tija, watoto hao ndio vijana wa baadae, ndio kichocheo kikubwa cha changamoto za upanuzi wa teknolojia “Mtoto ndio kijana wa baadae, ndio mletaji changamoto za maendeleo ya Tanzania na Afrika, mtoto akijengwa sasa atakuwa bora baadae katika ujana ila akiwa hajajengwa, atakuwa mwovu na si bora kama serikali na jamii zinavyohitaji, hivyo jamii na serikali tusimame kidete kwa pamoja kumjenga mtoto wetu katika maadili endelevu kama kaulimbiu inavyosema” alisema Katibu msaidizi.

Pia Katibu msaidizi alieleza kuwa “Serikali inapaswa kutafuta njia mbadala ikishirikiana vyema na jamii kutatua changamoto zinazomkabili mtoto, changamoto ni nyingi sana, hukwamisha ndoto za watoto wengi.”. Alitaja baadhi ya changamoto hizo katika malezi bora ya mtoto kuwa ni pamoja na adhabu kali, haki za mtoto, elimu, usawa wa kijinsia, fursa kwa watoto, upendo toka kwa wanajamii nakadharika, hivyo serikali ijaribu kupambana na haya kwa njia za kuelimisha jamii kuhusu mtoto kupitia majukwaa ya wazi (forums), kwa kufungua kampeni juu ya mtoto na hata sheria zitakazomwokoa mtoto kutoka katika mateso na changamoto za jamii.