UDINI NA UKABILA VINAITAFUNA NCHI YETU- MHE.LUCY OWENYA

 

Mjumbe wa Kamati kuu ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO ( CHADEMA) Godbles Lema pamoja na mbunge wa viti maalum mkoa wa Kilimanjaro Lucy Owenya wamnadi mgombea udiwani kata ya Machame Magharibi Wilayani Hai.

Akimnadi mgombea udiwani wa kata hiyo mh Lema amewataka wananchi wa kata hiyo kumchagua diwani kutoka CHADEMA kwakua ndicho chama kilicho na malengo ya kuleta maendeleo kwa wananchi na kutetea wanyonge bila ubaguzi.

Amewaambia wananchi kuiadhibu CCM kwa kuinyima kura kutokana na kitendo chao cha kuwanunua madiwani wa chama hicho kwa garama zitokanazo na kodi za wananchi.

Amesema uchaguzi huu unaofanyika katika kata 43 nchini, zinatumia mamilioni hela ambayo yangewasaidia wananchi katika sekta mbalimbali mfano afya, elimu pamoja na kuongeza mishahara kwa wafanyakazi.

Kwa upande wake mh Lucy Owenya, amewaambia wananchi wana sababu kubwa ya kumchagua mh Elibarck Lema kwakua maendeleo kwenye kata hiyo yametokana na juhudi zake mwenyewe wakati akiwa diwani kwenye kata hiyo.

Mh Lucy amewaambia wamchague mgombea huyo kutokana na hekima, juhudi na busara alizonazo .

Ameongeza kuwa mgombea huyo ana umuhimu mkubwa hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa linakabiliwa na mambo ya UDINI, UKABILA na uonevu unaonezwa na watawala dhidi ya upinzani na wanaharakati mbalimbali.

Mkutano huo wa ufunguzi umefanyika katika Kijiji cha Kyeeri kata ya Machame Magharibi.

Baadhi ya viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro Bazili Lema, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Hai Helga Mchomvu, diwani wa viti maalum Halmasha ya Wilaya Moshi Haika Lyatuu, madiwani wa Halmashauri ya Hai na viongozi mbalimbali wa Chama wa Wilaya Hai.
Mwisho.

Imeandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa viti maalum mkoa wa Kilimanjaro, idara ya habari na mawasiliano.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*