UCHAGUZI LIBERIA SASA KUINGIA DURU YA PILI.

 Mchezaji wa soka wa zamani wa Liberia George Weah na makamu wa rais Joseph Boake, wanaelekea duru ya pili ya uchaguzi kwenye uchaguzi wa rais nchini Liberia. 

Hii inakuja wakati matokeo yote kwenye uchaguzi wa siku ya Jumanne yamehesabwa, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi. 

Bw. Weah ambaye ni mwafrika wa kwanza kushinda tuzo la kandanda la Ballon D’Or, anaongoza kwa asilimia 39 huku Bw. Boakai akiwa wa pili kwa asilimia 29, Duru ya pili kati ya wawili hao inatarajiwa mwezi ujao.

Wanaongoza wagombea wengine 20 ambao wanataka kuchukua nafasi ya Ellen Johnson Sirleaf, mwanamke wa kwanza kuchaguliwa rais barani Afrika na mshindi wa tuzo la amani la Nobel, Weah na Boakai wote walikuwa wametabiri kuwa wangeshinda duru ya kwanza. 

Meneja wa zamani wa Bw. Weah akiwa mcheza kandanda, Arsene Wenger, mapema wiki iliyopita alipotoshwa na habari kuwa Weah tayari alikuwa amechaguliwa rais.