TSNP KUTOA MSIMAMO JUU YA MIKOPO YA WANAFUNZI KESHO

TSNP KUTOA MSIMAMO JUU YA MIKOPO YA WANAFUNZI KESHO

Kutokana na kauli iliyotolewa leo bungeni na Waziri wa Elimu Mh Joyce Ndalichako kuhusiana na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini, Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) tutakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari siku ya Jumamosi ya tarehe 11/November/2017.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa TSNP, Hellen Sisya imeeleza kuwa, mkutano huo unatarajia kufanyika katika hoteli ya Landmark iliyopp Ubungo Jijini Dar es Salaam.

Leongo la mkutano huo ni kwa ajili ya kutoa msimamo wetu kuhusiana na ubaguzi unaofanyika katika suala zima la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

Ewe mwanafunzi, mzazi,mlezi, kaka, dada tunakuomba utoe sapoti ya harakati hizi kwa kushare hash tag yetu ya *Loans4AllStudents* kwenye mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, Twitter na mitandao mingine yote ili kuunga mkono harakati hizi kwa ajili ya kulikomboa taifa hili kwa kuwekeza kwa vijana wa taifa letu kupitia Elimu.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*