TRUMP AENDELEZA MGOGORO NA VYOMBO VYA HABARI NCHINI MAREKANI.

Rais Donald Trump ameendeleza mgogoro wake na vituo vya runinga nchini humo akisema kuwa vimekuwana upendeleo na kuonya kwamba atafutilia mbali leseni zao.

Alikasirishwa na ripoti ya kituo cha habari cha NBC iliodai kwamba kwamba aliwaagiza maafisa wake wa usalama na majenerali kwamba alitaka kuongezwa kwa kiwango kikubwa silaha za kinyuklia nchini humo.

Rais huyo alisema kuwa habari hiyo ilitungwa.Waziri wake wa ulinzi Jim Mattis aliitaja taarifa hiyo kama isiokuwa ya ukweli.

Wiki iliopita NBC iliripoti kwamba waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alimuita bwana Trump ‘mtu mjinga’ matamshi ambayo Bwana Tillerson hajayapinga lakini ambayo rais Trump ameytaja kuwa habari bandia.

Wanahabari wanasema kuwa rais huyo atapata shida kufutilia mbali leseni za vyombo vya habari.Zinadhibitiwa na tume ya mawasiliano nchini humo.

Lakini baadhi ya makundi ya kupiganiahaki yanasema kuwa rais Trump anaweka mfano mbaya kwa viongozi wengine.

Chanzo:BBC.