TAMADUNI ZA NDOA ZA KUSTAAJABISHA, ANAE KATA KIPANDE KIKUBWA CHA KEKI NDIYE KIONGOZI WA FAMILIA

Wahenga walisema “Ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni’’ pia wengine wakasema “Kutembea kwingi kuona mengi” Kunatamaduni na sheria ambazo zinatumika kwenye nchi mbalimbali duniani, ambapo ukisikia unaweza ukabaki na bumbuwazi, kwasababu ukiziangalia ni tofauti kabisa na ulivyo zoea na wala haujawahi kuzani kama kuna tamaduni hizo duniani. Fuatilia tamaduni hizi za ndoa zinazo staajabisha na kufurahisha pia, kutoka nchi mbalimbali duniani:

 Ufaransa: Champagne kwenye bakuli la chooni

Wanandoa nchini Ufaransa kulingana na tamaduni za baadhi ya sehemu hutakiwa kula chocolate na kunywa champagne baada ya mapokezi, hilo sio tatizo, tatizo ni hii kuwa wanatakiwa kutumia bakuli la chooni kunywea champagne ambapo lengo la utamaduni huu ni kuwapa uimara na uvumilivu katika ndoa yao.

 Congo: Nimakosa kutabasamu siku ya ndoa

Ni jambo la kushangaza na kuajabisha lakini ni katika kutimiza mila na desturi, unaambiwa Bibi na Bwana harusi nchini Congo wanatakiwa kuiweka furaha yao kwenye mashavu, hawatakiwi kutabasamu siku nzima ya harusi na kama watafanya hivyo itachukuliwa kuwa hawakuwa serious kuhusu ndoa.

 Pakistan: Bwana Harusi kuibiwa viatu

Dada wa bibi harusi na ndugu wengine wa kike wanaruhusiwa kuiba viatu vya Bwana harusi na kama anavitaka lazima avikomboe kwa pesa ili virudishwe vikiwa salama.

Urusi:ilia Anayekata kipande kikubwa cha keki ndiye kiongozi wa familia

Wanandoa wapya Urusi wanatakiwa kuchangia mkate wa asili unaoitwa karavaya ambapo yeyote kati yao atakayekata sehemu kubwa ama mume au mke bila kutumia mikono ndiye atakuwa kiongozi wa familia.

Fiji: Jino la Papa kwa baba mkwe

Utamaduni wa ndoa katika nchi ya Fiji ni kuwa pale Bwana harusi anapoomba ruhusa kwa baba Mkwe ili ashikane na Mwanamke wakati wa ndoa lazima ampe baba mkwe huyo jino la papa.

 Mauritius: Bibi harusi lazima awe na uzito mkubwa

Katika ndoa za sehemu nyingi duniani, Mabibi harusi hufanya diet kurekebisha miili yao na kupunguza uzito kabla ya ndoa lakini sio hivyo kwa Mauritius, Wasichana wadogo wanalazimishwa kula ili waongezeke uzito wakati wa ndoa zao ambapo hii ni kwa sababu wanaamini kuwa Mwanaume lazima awe na uwezo wa kumlisha.

 Jamaica: Bibi harusi hupita mtaani

Hii inapatikana katika vijiji vya Jamaica ambapo wanakijiji hujipanga mstari barabarani kumuangalia Bibi harusi kwa lengo la kutoa maoni kuhusu muonekano wake ambapo kama watu wengi wataupinga, atalazimika kurudi nyumbani kubadilisha kisha arudi tena hadi pale wayakaposema anapendeza.