SIHITAJI KUFANYA MAAMUZI JUU YA HILI NIPO TAYARI, RAFAEL NADAL

Mchezaji tenis namba moja katika viwango vya ubora wa mchezo huo duniani, Rafael Nadal amesema yupo fiti kucheza michuano ya fainali ya ATP inayotarajiwa kuanza hapo kesho siku ya Jumapili huko London.

Mchezaji tenis namba moja katika viwango vya ubora duniani, Rafael Nadal

Mhispania huyo ambaye hakamatiki kwa sasa katika mchezo huo alishindwa kuendelea na michuano ya Paris Masters wiki iliyopita baada ya kufuatia kupata majeraha ya goti hivyo watu wengi kutazamia kama angeweza kushiriki mashindano haya ya mwisho wa msimu Jijini London.

Akizungumza na Sky Sports baada ya kuwasili London siku ya Jumatano, Nadal amesema “Nimefanya kilakitu ambacho ningehitaji kufanya ili kuwa tayari kwa mashindano ya London.”Amesema Nadal.

“Sihitaji kufanya maamuzi juu ya hili nipo tayari kucheza na nitajaribu kwa uwezo wangu wote.”

Nadal amekusudia kusalia katika nafasi hiyo ya kwanza ya viwango vya ubora wa mchezo wa tenis duniani, huku kesho akishuka dimbani katika michuano hiyo ya fanali ya ATP inayotarajiwa kumalizika Novemba 19 ya mwaka huu.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*