SERIKALI YALALAMIKIA MAAMUZI YA KENYA KUZUIA KUUZWA KWA MITUNGI YA GESI ZA KUPIKIA ZINAZOTOKA TANZANIA.

Na Jyross Curtis

Kufuatia hatua iliyochukuliwa na serikali ya Kenya kupiga marufuku gesi ya kupikia toka Tanzania kuuzwa nchini humo hivyo serikali ya  Jamhuri ya Muungano ya Tanzania imelalamika Kufuatia wafanyabiashara wa Tanzania kusimamishwa kuuza gesi ya kupikia nchini humo.

Mathalani malalamiko hayo yamebainishwa na katibu wa kudumu wa wizara ya biashara na uwekezaji Profesa Adolf Mkenda kuwa serikali imegundua katazo hilo kupitia vyombo vya habari mjini vya Nairobi kwamba Kenya imepiga marufuku uingizwaji wa gesi ya kupika kutoka Tanzania kupitia mpaka wa Kenya na Tanzania.

Katibu wa kudumu wa wizara ya biashara na uwekezaji Profesa Adolf Mkenda

Prof Mkenda ameeleza kuwa kitendo kinachofanywa na Kenya ni  kinyume na makubaliano ya jumuiya ya Afrika mashariki na makubaliano yaliyoafikiwa baina ya Kenya na Tanzania . Katazo hilo toka Kenya lilitolewa mwezi Mei 18, 2017.

Aidha amesema  hatua hiyo ya Kenya itaathiri wafanyibiashara  na raia wa kawaida wanaoendesha maisha yao  kupitia biashara ya kuuza gesi hata hivyo itasababisha mgongano wa kimakubaliano katika jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Ripoti inaeleza kuwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika mashariki ambao ulifanyika mwezi juni 2- 2017 na hivyo kukutanisha pamoja  mawaziri wa biashara na viwanda, ulisema kwamba Kenya ilifaa kuondoa marufuku hiyo ili kukubaliana na makubaliano hayo ya Afrika mashariki.

Hivyo basi Profesa Mkenda amesema kuwa serikali ya Tanzania  itaendelea na mpango wa kutatua tatizo hilo na hivyo wafanyabiashara wawe na uvumilivu tu.