SAUTI YA GHETTO ILIVYOTEST MITAMBO.

Na: Richard Samwel


Yalitumika masaa 38 na dakika 45 kushuhudia hitimisho la vita fupi zaidi kuwahi kupiganwa katika mgongo wa ardhi.


Naam vita baina ya vikosi vya sultan wa Zanzibar na vikosi vya uingereza mwaka 1896 kunako tarehe 27 ya mwezi August, inabakia kuwa vita iliyopiganwa kwa muda mfupi zaidi katika uso  wa dunia. 

Katika mwili uliojengeka kimazoezi  na uliobeba kiwiliwili chenye umbo la  mwanaume wa shoka,mwili wenye nakshi za michoro ya tatoo,
Katikati ya tatoo nyingi katika bega  lake la  kulia,upo mchoro wa tatoo iliyobeba sura ya Mwanamke. Naam tatoo hiyo ni ya mwanamama  Jacqueline Pardo,mama yake mzazi.

Akiwa na umri wa miaka 15 alimuahidi mama yake mzazi atamfanya  kuwa malkia,kauli hii nzito ilionyesha kuchoshwa kwake na maisha ya gheto yaliyokuwa  yamezungukwa na Umaskini mkubwa.

Akiwa ameanza kuyapigania maisha yake tangu akiwa na umri wa miaka mitano Mara baada ya baba yake  kuwachomea kitanda kwa ulevi na kutokomea.

Soka lilikuwa tumaini pekee la  kuyaokoa maisha yake na kuiokoa familia yake.Mapenzi yake na juhudi katika soka vilimfanya muda wote awe amejaa vumbi katika mazoezi hali iliyopelekea apewe jina la  utani la  mla mavumbi,ama Cometierra kwa lugha yake mama.

Wakati anasajiliwa na timu ya Colo Colo,mshahara wake wa kwanza, aliuchukua kisha kwenda kwa mama yake na kumwambia,
` mama tunaenda supermarket, tutanunua kila tu,`

Haya yalikuwa matunda yake ya awali katika soka,Mara ya pili usajiri wake wa kuelekea Bayern Leverkusen, ulimfanya alie kwa uchungu kwa mama yake akimwambia mama yake,kuwa mama tumekuwa  milionea.

Huyo ndo Arturo Vidal mtoto wa gheto ambaye kwake soka ni mkombozi.

Katika soka lake la  shoka,na juhudi na kizazi cha watoto wenzake wa gheto, Wameliwezesha taifa lao la  Chile kutwaa ubingwa wa copa  America Mara mbili mfululizo, kitu ambacho wachile walikisubiri kwa miongo kenda  na miaka Tisa.

Baada ya kushindwa kufuzu kushiriki kombe la  dunia litakalofanyika huko urusi mwaka 2018,Arturo Vidal alitangaza kustaafu kuitumia  timu yake ya taifa ya Chile.
Katika umri wa miaka 30 hakika uamuzi huu ulichagizwa na uchungu wa kuikosa  nafasi hiyo,zilikuwa ni hasira na uchungu tu.

Nani ameusahau ule msemo wa wamarekani usemao kuwa,

`you can take the nigger out of the ghetto, but you can’t take the ghetto of the nigger`.
Waswahili pia hupata kusema kuwa,Jasiri haachi Asili,
Niliposoma uamuzi wa Arturo Vidal kustaafu kuchezea timu yake ya taifa Katika umri wa miaka 30 sikutaka kuidanganya akili yangu kuamini kuwa uamuzi huo utadumu.

Jasiri anaacha vipi asili yake?
Katika umri wa miaka 12 baada ya kusajiriwa na klabu ya Colo Colo,katika mkataba wake kulikuwa  na kipengele kilichomzuia kuichezea timu yake ya awali ya Rodelindo.

Lakini Mara nyingi sana alikuwa akikivunja kipengele hicho kwa kuichezea timu yake hiyo ya mtaani,
Leo hii akiwa na medali mbili za ubingwa wa kombe la  copa  America,na Katika kiwango chake cha ubora wa soka angewezaje kuvumilia kuitazama timu yake ya taifa ikipambana uwanjani na yeye akiwa jukwaani?
 Nani kasahau kizazi hiki cha gheto cha Chile kilichomfanya Lionel messi atangaze kustaafu soka?

Kama ambavyo jasiri asivyoacha  asili,Arturo Vidal ameshatangaza kufuta uamuzi wake huo na kurudi kupambana katika timu yake ya taifa.
Watoto wa gheto ni wapambanaji na wapiganaji haswaa,Mtoto wa ghetto amerudi kundini kupambana kiume.