RONALD AIBUKA KIDEDEA TUZO FIFA.

Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wadunia wa Fifa 2017 baada ya kuwapiku wachezaji Lionel Messi na Neymar katika kipengele hicho.

Tuzo hizo zimetolewa Oktoba 23 ambapo mchezaji huyo aliyeambatana na mpenzi wake na mwanae amewashukuru waliompigiakura kwa kuweza kushinda pamoja na mashabiki na wachezaji wenzake.

“Nashukuru wote mlionipigia kura kwa kunifanya nishinde tuzo hii,” amesema Ronaldo.

Mbali na tuzo hiyo Ronaldo ametajwakatika kikosi bora cha mwaka 2017 ambacho kimewajumuisha Messi na Neymar na nyota wengine akiwemo Sergio Ramos, Toni Kroos, Andres Iniesta, na Dani Alves.

Tuzo ya mchezaji bora wa kike wa Fifa 2017 ilienda kwa Lieke Martens ambaye hakuudhuria katika utoaji watuzo kutokana na kujiandaa na kujiandaa na mechi ya kufuzu kombela dunia la wanawake.

Ukumbi ulilipuka kwa shangwe wakati linatangazwa goli bora la mwaka ‘Puskas’ ambapo katika magoli 10 bora mashabiki walisikika wakimtaja nyota wa Arsenal, Olivier Giroud ambaye alitangazwa kama mshindi.

Wengine walioshinda tuzo za Fifa 2017 ni Zinedine Zidane (Kocha bora kwa waume), Sarina Wiegman (kochabora kwa wanawake) Gianluigi Buffon (Kipa bora), Mashabiki wa Celtic (Kikundi bora), Francis Kone (Mchezo wa kiungwana).