REKODI ALIZOWEKA LUKAKU BAADA YA USHINDI WA MAN U JANA

Manchester United wamepata ushindi wa mabao 4 – 0 hio ni habari, lakini habari kubwa ni kwamba ushindi huo umewafanya Manchester United kuwa klabu ya kwanza kutofungwa nyumbani mechi 250.

Ina maana katika mechi zote Manchester United walizocheza Old Trafford  kuna mechi 250 ambazo nyavu zao hazikuguswa na mpira wa wapinzani na inakua timu ya kwanza kufikisha rekodi hiyo huku Chelsea wakifuatia na Clean Sheet ya michezo 221.

Lakini Lukaku bao lake la leo ilikuwa bao lake la 90 katika Epl huku mabao 68 akiwafungia Everton, akiwafungia West Brom mabao 17 na 5 yaliyobaki amewafungia Manchester United, sasa anaungana na Robie Fowler, Wayne Rooney na Michael Owen kufikisha idadi hiyo wakiwa na miaka isiyozidi 24.

Si hayo tu bali pia Louis Saha na Robin Van Persie ndio wachezaji ambao wamewahi kufunga mabao 5+ katika michezo yao mitano ya mwanzo kuichezea United na goli la Lukaku linamaanisha ameifikia rekodi ya magwiji hao. Sasa Lukaku anakuwa sawa na Kun Aguero kama vinara wa ufungaji huku wote wakiwa na mabao 5.