RC MAKONDA AVIASA VYAMA VYA USHIRIKA KUANZISHA VIWANDA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Paul Makonda leo amezindua Jukwa la Ushirika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amevitaka Vyama vya Ushirika kuwekeza kwenye Viwanda vidogovidogo.

Mheshimiwa Makonda amesema kuwa hatua za Vyama hivyo kuwekeza katika Viwanda itasaidia kuinua Uchumi wa Vyama na Wanachama wake.

Amesema
Wananchi wengi bado hawajaelewa umuhimu na nguvu ya Ushirika ndio maana baadhi yao bado ni Maskini hivyo amewaasa Wananchi kujiunga kwenye Vyama vya Ushika ili kumiliki uchumi.

Aidha RC Makonda ameviasa vyama hivyo kuzingatia sheria, kanuni na tatatibu za kuanzishwa kwake ili kufikia malengo.

Miongoni mwa Changamoto zilizotajwa kufifisha nguvu za Ushirika ni pamoja na Makato makubwa ya Fedha, Kucheleweshwa kwa Marejesho, Wakopaji kushindwa kulipa madeni na kukimbilia kuweka zuio la kufilisiwa mali Mahakamani na Baadhi ya Waajiri kutowasikisha makato na marejesho ya Wanachama waliokopa.

Kuhusu Changamoto hizo RC Makonda amewataka Viongozi kuziandika Changamoto hizo kisha kumpatia ili aziwasilishe kwenye ngazi husika ili zipatiwe utatuzi.

Katika hatua nyingine Makonda ameviomba vyama vya Ushirika kumuunga mkono katika kampeni ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu kwa kumchangia Saruji na vifaa vingine ambapo vyama hivyo vimeahidi kumuunga mkono kwakuwa kampeni hiyo ni njema na inalenga kuboresha elimu na ufaulu wa Wanafunzi.

Mkoa wa Dar es salaam una jumla ya Vyama 763 vyenye wanachama zaidi ya 238,897 ambapo kila mwanachama akijitolea mfuko mmoja wa Saruji itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya ukosefu wa Ofisi za Walimu.