RC MAKONDA APOKEA TANI 405 ZA NONDO NA MIFUKO 500 YA SARUJI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amepokea zaidi ya Tani 405 za Nondo kutoka kiwanda cha AM Steel and Iron Mills Ltd na Mifuko ya Saruji 500 kutoka Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa LAPF kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari Dar es Salaam.

Nondo hizo zenye thamani ya zaidi ya Shillingi Million 150 zimetolewa kama utangulizi ambapo Kiwanda hicho kimesema kitatoa Nondo za kujenga ofisi zote 402 za Walimu.
Akipokea Nondo hizo RC MAKONDA ameshukuru kiwanda hicho kwa kuunga Mkono kampeni hiyo inayolenga kurejesha heshima kwa walimu na kuwapa morali ya kufanya kazi ili kuleta matokeo chanya kwa Wanafunzi.
Wakati huohuo Mfuko wa hifadhi ya Jamii LAPF umemkabidhi RC MAKONDA Kiasi cha Shillingi Million 5 kwaajili ya kununua Mifuko 500 ya Saruji za Ujenzi wa Ofisi za Walimu.
RC MAKONDA amewahimiza Wananchi na wadau kuendelea kuchangia kampeni ya ujenzi wa Ofis za walimu kupitia Saruji, Kokoto, Mchanga, Nondo Mbao, Milango, Madirisha na Bati ili kufanikisha kampeni hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda hicho *Shekh SHAHID SALIM amesema watatoa kiasi chote cha mahitaji ya Nondo zinazohitajika kwakuwa wanatambua umuhimu wa Walimu na kazi kubwa anayoifanya RC MAKONDA kwenye Mkoa wa Dar es Salaam.
Nae Meneja Masoko na Mawasiliano LAPF Bwana JAMES MLOWE amesema kuwa wameamua kumuunga mkono RC MAKONDA kwakuwa fedha zinazotolewa kwake zinafanya kazi iliyokusudiwa.
Tayari kasi ya ujenzi wa Ofisi za walimu inaendelea katika Shule mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*