RC MAKONDA AFANYA KIKAO NA TANESCO, AWAGIZA KUTATUA KERO ZA UMEME KWA WANANCHI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo amefanya kikao na Mameneja wa TANESCOnKanda zote za Dar es Salaam kujadili mkakati wa kumaliza tatizo la kukatika kwa umeme na maboresho ya miundombinu ya Umeme.


Lengo la kikao hicho ni kujadili mahitaji ya Umeme kwa Mkoa, Kero ya kukatika umeme mara kwa mara (Mgao), Mpango Mkakati wa kukabiliana na Madhara yatokanayo na Mvua zinazoendelea kunyesha na Mpango mkakati wa kuhakikisha Taasisi zote za Umma ikiwemo Shule, Vituo vya Polisi na Vituo vya Afya vinakuwa na Umeme wa Uhakika.


RC MAKONDA amesema kuwa kukatika kwa umeme imekuwa kero kubwa kwa wananchi na wakati mwingine kusababisha hasara hivyo anaamini TANESCO ya sasa chini ya Serikali ya awamu ya Tano itamaliza kero hizo.


Katika kikao hicho TANESCO wamemuahidi RC MAKONDA kuwa Umeme utaongezeka kuanzia leo Maeneo yote yaliyokuwa yakisumbuliwa na upatikanaji wa Umeme hali itakuwa Shwari kuanzia leo.


Kuhusu suala la Umeme mashuleni wamekubaliana kuandaa mchanganuo wa mahitaji yanayohitajika kisha kufikisha ofisini kwake ili kila shule iunganishwe na huduma ya umeme.


RC MAKONDA amewataka kuwa na lugha nzuri kwa wateja na kufika kwa wakati pindi wanapopewa taarifa za hitilafu ya umeme.


Kwa upande wake Meneja mwandamizi TANESCO Dar es Salaam na Pwani Eng.MAHENDE KUGAYA amemuahidi RC MAKONDA kuwa watatekeleza yale yote waliyoagizwa kuanzia siku ya leo ikiwemo kutatua kero za Wananchi za mgao wa Umeme na kufikisha huduma ya umeme kwenye Taasisi zote za umma ikiwemo Vituo vya Polis, Vituo vya Afya na Shule.


Aidha amemuhakikishia RC MAKONDA kuwa eneo la Mbagala na Kigamboni kuanzia mwezi Disemba watapata umeme wa uhakika.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*