Rais Magufuli akagua sukari kabla ya kufungwa kwenye mifuko

darmpya:Kitaifa#Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sukari kabla ya kufungwa kwenye mifuko yake alipotembelea kiwanda cha sukari cha Kagera kilichopo Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera Novemba 8, 2017.

Aliagiza viwanda vyote vya kuzalisha sukari nchini kutafuta namna ya kuongeza uzalishaji ili kumaliza tatizo la upungufu wa tani 130,000 unaoikabili nchi kwa sasa.

Aidha, alimpa siku tatu Waziri wa Kilimo Tanzania Dkt Charles Tizeba kuwaondoa mara moja maafisa wote waliokuwa wakitoa vibali kwa waingizaji wa sukari nchini humo kutokana na vitendo vyao vya kutoa vibali hovyo na hivyo kudhoofisha viwanda vya ndani.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*