RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WATENDAKAZI WAPYA WA SERIKALI

 

 

Na Jyross Curtis

 

Taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu kupitia kwa naibu mkurugenzi wa maawasiliano ya Rais bwana Jaffar Haniu imesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Mei, 2017 amewaaapisha watendaji wa serikali ambao watafanya kazi kwa weredi katika nyadhifa walizoteuliwa na Rais wa Jamhuri.

 

Watendaji hao wapya wa serikali walioteuliwa ni pamoja na Bw. Tixon Tuyangine Nzunda ambaye Mh. Rais amemteua kuwa naibu katibu mkuu, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) atayeshughulikia masuala ya elimu.

 

Viongozi wengine walioapishwa na Mhe.Rais Dkt. Magufuli ni pamoja na Bwa. Rajab Omar Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Bw. Bernard Mtandi Makali ameapishwa kuwa katibu Tawala Mkoa wa Rukwa pia amemteua Bw. Clifford Katondo Tandari, kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro na Rais amemuapisha Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

 

Aidha viongozi wote walioapishwa na Mh. Rais wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuwaletea wananchi maendeleo chanya katika jamii zao.

Hafla ya kuapishwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na viongozi mbalimbali wa Serikali.