POLEPOLE AZUNGUMZA BAADA YA K IKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA.


Katibu wa Itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo na wanahabari, Polepole ameleza yaliyofikiwa na halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) iliyokutana leo katika kikao chake.
“Chama Cha Mapinduzi kimefanya uchaguzi wake kwa mafanikio makubwa sana. Mashina ya chama yamehimarika , kwa nchi nzima CCM inamashina zaidi ya elfu 23 kote Tanzania.” Alisema Hamhrey.
Pia aliendelea kuharifukwamba uchaguzi umekamilika kwa kwa zaidi ya 97% katika wilaya 161 Tanzania, NEC imeridhia kuelekeza wilaya zifuatazo zitatangaza upya nafasi za uwenyekiti, wilaya hizo nipamoja na Moshi mjini, Siha, Hai, pamoja na Makete, katika wilaya hizo zilizo tajwa, NEC imeridhia kwamba wagombea waliokua wamejitokeza walikua wanakasoro za kimaadili na kikanuni na hatahivyo walikua na viashilia hatari kwa chama.

NEC imetoa maelekezo kuwa wilaya ya musoma itaundwa kwa wilaya mbili za kichama yaani Wilaya ya kichama ya Musoma mjini na Wilaya ya kichama ya Musoma vijijini. Kwa uamuzihuo inamaanisha kwamba uchaguzi wa viongozi wa wilaya na jumuiya zitztangazwa upya.

Hatahivyo NEC iliendelea kukumbusha kuwa wale wote walioteuliwa kushiriki chaguzi za chama kwenye wilaya mbalimbali, waomba dhamana hao halihaswa na bwana Polepole, kuwa wanapaswa kuzingatia kanuni na maadili za uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi. Aliendelea kwakutoa onyo kuu kwamba, Chama kitafuta chaguzi zitakazo kua zimekiuka miiko na kanuni za Chama Cha Mapinduzi.

Pia ndugu Polepole alikemea swala lakujilimbikizia vyeo, aliwaasa wagombea kuwa wanapaswa kutokua na cheo zaidi ya kimoja , kwa wale watakao ewa nafasi kwenye ngazi ya wilaya watapaswa kuachia nafasi za chini walizo nazo.

Rushwa imekua ni moja wapo ya hoja katika mkutano huo, NEC imeamua kupambana na rushwa vilivyo kwenye uchaguzi wa CCM kwakuwakanya wagombea na kuwasisitiza wasijaribu kufanya vitendo vya rushwa kwasababu nimoja ya sababu kuu za kumpotezea mgombea sifa ya kugombea.

Ndugu Polepole aliendea kuwataarifu wagombea kwa kupitia wanahabari kuwa NEC itawaruhusu wagombea watakao kua wanahisi hawajatendewa haki, watatakiwa kukata rufaa kwa mujibu wa kanuni za uchazi wa CCM kifungu namba 28 inayo zungumzia malalamiko ya uchaguzi, kabla ya uchaguzi au baada ya uchaguzi.

NEC inakemea vikali kwa wale wanao anza kufanya kampeni kabla ya wakati, na bwana Humphrey Polepole alimaliza kwakuwasii wagombea kutofanya kampeni kabla ya wakati kwani watakua wamepoteza sifa ya ugombea.