PANYA WAHARIBU OFISI YA RAISI NIGERIA.

Raisi wa Nigeria Mohammed Buhari ametangaza kufanya kazi zake za ofisi akiwa nyumbani kwa muda wa siku 21 baada ya ofisi yake kuharibiwa na panya.

Buhari ameeleza hayo baada ya kurejea nchini kwake akitokea Uingereza alipokua akitibiwa kwa takribani miezi mitatu na siku kumi.

Aidha Raisi Buhari amewatoa hofu wananchi wake kwa kuwahakikishia kua hatua ya kufanyia kazi za kiofisi nyumbani kwake haitaathiri utendaji wa kazi kwa namna yoyote mpaka pale ofisi yake itakapokua sawa.

Hata hivyo baadhi ya wanaharakati na raia kadhaa kupitia mitandao ya kijamii wamekosoa hatua ya raisi Buhari kushindwa kuzungumzia maendeleo na afya yake kwa ujumla wakati akitoa hotuba yake kwa taifa siku ya jumatatu.