P-SQUARE KUPIGA MNADA JENGO LAO LA KIFAHARI LAGOS.Huenda siku za usoni tukasahau kabisa kama kulikuwa na kundi la muziki la P-Square kwani kwa sasa mapacha hao wanaanza kuuza baadhi ya assert zao ambazo walikuwa wanamiliki wote kwa pamoja kipindi wakifanya muziki kama kundi, Baada ya taarifa kusambaa kuwa wawili hao wanapiga mnada jumba lao la kifahari lililopo jijini Lagos, Nigeria.

Square Ville

Taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari  nchini Nigeria zinaeleza kuwa wawili hao wamefikia hatua ya kupiga mnada nyumba hiyo iliyopo eneo la Ikeja, jijini Lagos ili kila mmoja aweze kumiliki vitu vyake na hii inakuwa ni hatua ya kwanza tangu watangaze kundi hilo kusambaratika.

Nyumba hiyo ya kifahari waliyoipa jina la ‘SquareVille’ inauzwa kwa Naira milioni 320 sawa na bilioni 2 za kitanzania.

Tayari jumba hilo limeshawekwa lebo ya kuuzwa mbele ya geti tangia jumatano ya wiki hii ingawaje mpaka sasa wahusika wamegoma kuzungumzia ishu hiyo lakini kampuni LIB ambayo ndiyo inahusika na upigaji mnada wa nyumba hiyo imethibitisha hilo.

Nyumba hiyo ambayo ina vyumba 16 na swimming Pool ilijengwa mwaka 2010 ambapo kundi hilo lilitangaza wazi kuwa kiwanja tu cha mjengo huo kiliwagharimu Naira milioni 100.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*