ODINGA AZIDI KUONYESHA MSISITIZO JUU YA KUSHIRIKI UCHAGUZI .

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, umesisitiza kuwa hautashiriki katika Uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 26 mwezi huu.

Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga amesisitiza hilo katika mkutano wa hadhara mjini Mombasa Pwani ya nchi hiyo baada ya kurejea nchini, akitokea nchini Uingereza sikuya Jumapili.

Odinga aliyetangaza wiki iliopita kujiondoa kwenye Uchaguzi huo, amewaambia wafuasi wake kuwa Uchaguzi huo hautafanyika kwa sababu Tume ya Uchaguzi haijafanya marekebisho kama ilivyoagizwa na Mahakama ya Juu iliyofuta matokeo ya urais mwezi Agosti.

Pamoja na hio, muungano huo umetangaza kuwa maandamano ya amani, kushinikiza mabadiliko ndani ya Tume ya Uchaguzi yataendelea wiki ijayo, kila siku kuanzia siku ya Jumatatu hadi Ijumaa.

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya ndani imepiga marufuku katikati ya miji ya Kisumu, Nairobi na Mombasa kwa kile ilichosema kuwa waandamanaji wa upinzani wanatumia maandamano hayo kupora mali ya watu.

Hata hivyo, upinzani umesema utaendelea na maandamano hayo katikati ya miji hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto wamesema licha ya maandamano na shinikizo za NASA wataendelea na maandamano, uchaguzi utaendelea.

Tume ya Uchaguzi inasema iko tayarikwa Uchaguzi huo.