MUME AJINYONGA BAADA YA KUMNYONGA MKEWE HADI KUFA KISA WIVU WA MAPENZI.

Mkazi wa Misungwi, Kwilokeja Boniface (35) amemuua mkewe Shija Luchagula (30), kwa kumnyonga kisha na yeye kujinyonga kwa kile kinachodaiwa wivu wa mapenzi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana Jumatatu kuwa tukio hilo lilitokea jana katika kijiji cha Mwiligiligili wilayani Misungwi.
Alisema mwanaume alitoka shambani akakuta tairi nyingi zabaiskeli kwenye uwanja wa nyumba yake ndipo ukazuka ugomvi baina yao akimtuhumu mkewe kutokuwa mwaminifu kwenye ndoa yao hivyo alianza kumpiga kwa fimbo kisha kumnyonga mpaka akafariki dunia.
Alisema baada ya kufanya hivyona yeye alichukua jukumu la kujinyonga kwa kamba ili kukwepa mkono wa sheria.
“Kwa sasa polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na vifohivyo na miili ya marehemu tayari imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi”