MTAZAMO WAKO NDIO FIKRA ZAKO

Chacha G,

Fikira zako ndio siraha pekee ya kuweza kukufanya ukaamua na kutenda kitu chochote kile, Fikira zako ndio kitu pekee cha kuweza kukusaidia katika kupanga na kutenda na kufikia malengo ya ndoto zako . Nafasi nyingi zimepotea kwa sababu ya kitu kinachoitwa Fikira , kwa watu wenye Fikira chanya, Fikira hizo huwa ni mtaji na siraha katika kufikia “mafanikio” kwa watu wenye Fikira hasi, Fikira hizo ni sawa mabonde, milima, ukuta wa kuzuia mafanikio yao, 
Ebu tujiulize ni Mara ngapi umeskia watu wakisema siwezi na hawamini katika kuweza? Unaposema siwezi kufanya (I can’t do) hapa kuna mambo mawili

Unasema huwezi kwa sababu, hujui namna ya kufanya au hutaki kufanya na kama Unasema huwezi kwa sababu  “huwezi kufanya “hicho ni kitendo cha kujifunza na kuaamua kufanya na kama” huwezi ” kwa sababu ya Fikira zako hili ni swala la kubadili Mtazamo na kuwa na Mtazamo chanya Kuhusu hicho kitu na kuamua kufanya

Swali, je Fikira zetu tunazaliwa nazo au tunazipata katika makuzi yetu na ni kwanini watu wengine wawe na Fikira chanya na wengine wawe na hasi kulingana na jamii inavyoweza kuzitafasiri?

Fikira za mtu yeyote znaweza kubadilika kutokana na sababu mbali mbali hapa kuna mambo makuu mawili znaweza kubadilika kutoka Fikira hasi kwenda Fikira chanya au kinyume chake sababu ambazo znaweza kusababisha mbadiliko huu ni hizi zifuatazo:

-mazingira
-mazoea
-elimu
Tunapoongelea mazingira hapa tunajumisha nyumbani malezi yako, shuleni, kazini, vyombo vya habari (media), utamaduni wa jamii husika, dini na mazingira ya kisiasa.

Mazoea, tabia na Fikira za watu mbalimbali hubadilika kulingana na mazoea na watu, matukio katika maisha yetu ya kila siku, tukiwa na mazoea na watu wenye mitazamo chanya katika mambo yao ya kijamii, kisiasa na kiuchumi na Fikira zetu pia zitakuwa chanya na kinyume chake pia
Elimu, hapa naongelea elimu zote mbili elimu rasimi na elimu isiyo rasimi (formal and informal education) hapa siogelei tu vyeti vya ufaulu (academic qualifications) elimu ni hekima ambayo itakufanya uweze kufanikiwa na kutenda na kugundua mambo mbalimbali katika jamii na kuleta mafanikio katika jamii husika, elimu haitufundish tu namna ya kutengeneza maisha bali inatufundisha namna ya kuishi, kwa mtu yeyote atakayepata elimu bora kati ya hizo mbili atakuwa na Fikira chanya katika mambo yake na kinyume chake pia inawezekana..,
Utagunduaje mtu mwenye Fikira chanya? Kuwa na Fikira chanya ni kama mtu mwenye afya bora asiyekuwa na ugonjwa wowote mtu Huyo ni kama tunda ambalo halina msimu, ni rahisi sana kumgundua, anajali, anajiamini, mvumilivu, Ana matarajio makubwa kwake na kwa wengine, anajituma, anatatua matatizo, mwaminifu watu hawa wapo katika jamii na baadhi ya watu ndani ya jamii husikika wakiwatolea mifano na kusahau kuwa na wao wakiamua wanaweza kuwa zaidi ya hapo

Kwanini watu hugundua wana mitazamo hasi lakini hawataki kubadilika?
Utakubaliana na mimi kwamba mtu anaweza kugundua mimi ni mwizi, mlevi, msinzi n.k na akaafiki kabisa vitu hivi ni vibaya na vinaharibu maisha yangu au kuyarudisha nyuma lakini inakuwa ni vigumu kubadilika, katika uhalisia wa binadam hupingana na mbadiliko haijalishi unatoka pazuri kwenda pabaya au pabaya kwenda pazuri lazima utajiskia haupo sawa (uncomfortable) mapokeo haya yanaitaji mda na uvumilivu ili uweze kuishi vizuri kwenye mfumo mpya ulio hamia.

Ila inawezekana kabisa kubadili Fikira zako kutoka kwenye Fikira hasi kwenda chanya endapo tu
Utagundua wewe ni wewe na hakuna mwingne anaweza kufanya kama wewe, ubaini na kutambua kwamba unafikira hasi na zinahitaji mbadiliko, kuwa na hamu ya kuwa na Fikira chanya, kubadili mitazamo na kutazama yale mazuri na kujifunza, kuwa na tabia ya kufanya vitu kwa mda na kujizuia kujidanganya kwamba nitafanya, jiamini na simamia unachokiamini hata kama ni kigum kwa kias gani, usiache kujifunza mambo mbalimbali kwa kusoma vitabu mbalimbali au kupitia watu.

Nipende kufanya hitimisho kwa kusema kwamba Fikira zetu ndizo utumwa wetu au uhuru wetu kwa kutegemea aina za Fikira tulizo nazo vichwani mwetu kwa maana ya kwamba Fikira hasi au chanya..

“Badili Fikira zako kubadili maisha yako (change your attitude to change your life “