MRISHO GAMBO: WATU KUHAMA VYAMA NI SUALA LA KAWAIDA, UPINZANI ACHENI POROJO.

Mkuu wa mkoa wa Arusha bwana Mrisho Gambo ameeleza kwamba suala la watu kuhama vyama kutoka chama kimoja cha siasa kwenda kingine ni suala la kawaida na halipaswi kutumika kama mtaji wa kisiasa.


Gambo ameeleza hayo kufuatia madai ya hivi karibuni ya wabunge wa upinzani kudai kumekuepo na viashiria vya rushwa katika sakata la madiwani wa vyama hivyo kujiudhuru na kuhamia chama tawala hali iliyomlazimu Gambo kutolea ufafanuzi.
“Hao madiwani wengi wao walikua CCM kabla ya kwenda kugombea kupitia chadema, je hapo napo walilipwa shingapi?” Alieleza Gambo.

Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kwamba viongozi na wawakilishi kutoka vyama pinzani wanawajibika kutekeleza yale waliyoahidi wapiga kura wao na kuachana na porojo ambazo haziwezi kuwasaidia wapiga kura wao.

Gambo pia ameeleza dira yake kiuongozi kwa mkoa wa Arusha ni kuwaletea maendeleo wana Arusha na si vinginevyo kwani wana Arusha wanahitaji zaidi maendeleo kuliko majibizano ya kisiasa.