MR. NICE:SHOO ZA BONGO ‘MICHOSHO’

MKALI wa Miondoko ya Tanzania, Kenya na Uganda (Takeu), Lucas Mkenda ‘Mr. Nice’ amefungukia sababu za kususa shoo ndani ya Bongo, ni kwa sababu ya mapromota na waandaaji wa shoo hawanapesa za kumlipa ndiyo maana hawezi kufanya.

Akichonga na Mikito Nusunusu, Mr. Nice alisema ingawa anapiga shoo nyingi nje ya Bongo, nchini ana muda wa miaka minne mpaka sasa hajafanya shoo yoyote kwa sababu tu ya kushindwana na mapromota.

“Unajua kwa mfumo wa mapromota wa ndani, kiukweli hakuna wa kuweza kuandaa shoo na kunilipa, ndiyo maana nimeamua kuzipa kisogo shoo za ndani na nina dili na shoo zanje tu,” alisema Mr. Nice.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*