MKUU WA MKOA AAGIZA MIFUGO YOTE LAZIMA IWEKWE ALAMA

Asema uwekaji wa alama mifugo ni kwa mujibu wa sheria namba 12 ya mwaka 2010. Hayo ameyasema leo katika uzinduzi wa zoezi la uwekaji alama mifugo Wilaya ya  Mbarali jumla yA ng’ombe 197,049 wana yatakiwa kuwekwa alama.

Amesisitiza atakayepuuza kuwekewa mifugo yake alama mpaka tarehe 14 /8/2017 atakuwa amekiuka sheria na hatua Kali zitachukuliwa.

utiaji alama utasaidia kudhibiti wizi wa mifugo, magonjwa ya mifugo, uingizaji mifugo kiholela na zaidi itasaidia kuwa na matumizi bora ya ardhi na hivyo kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji.

Amewaonya baadhi ya wafugaji wanaoingiza ngombe eneo la Ihefu na Hifadhi ya Ruaha wakati wa usiku waache mara moja.

Aidha amewataka viongozi wa vijiji kuacha kuwaonea wafugaji ambao wameiishi nao muda mrefu lakini zoezi hili limeanza wameanza kuwafukukuza.