MKURUGENZI WA MAWASILIANO WHITE HOUSE ATUMBULIWA NA TRUMP SIKU 11 TANGU ATEULIWE

Rais wa Marekani Bwana Donald Trump amemtumbua mkurugenzi wa mawasiliano wa ikulu ya white house Bwana Anthony Scaramucci baada ya siku  11  tangu amteue.

Bwana Scaramucci aliteuliwa tarehe 21/7 mwaka huu kushika nyadhifa hiyo huku sababu ya kuondolewa kwake ikidaiwa ni shinikizo kutoka kwa Mnikulu mpya Bwana John Kelly.

Hatua ya kutumbuliwa kwa Bwana Scaramucci kumeshtua watu wengi wa Marekani haswa ikizingatiwa kwamba tarehe rasmi ya aliyopaswa kuanza kazi ni tarehe 15 August ,kwa maana hiyo Scramucci ametumbuliwa huku akiwa hajaanza rasmi kazi yake.