MHE ANTHONY MAVUNDE ATOA MAHUBIRI KWA VIJANA MTWARA

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe ANTHONY MAVUNDE amezindua Mafunzo ya UTAMBUZI WA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI kwa Vijana 847 kutoka Mikoa ya Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, na Dar es Salaam mafunzo yaliyozinduliwa Mkoani Mtwara.

Mhe Mavunde amewataka Vijana kuchangamkia fursa wasisubiri serikali itoe matangazo, iwatafute, iwakusanye, iwape ujuzi
Msingi wa maisha ya kijana unaanzia hapa
Kijana wa kitanzania jiamini, timiza wajibu wako

Ombi kwa vijana
Vijana waliopata fursa ya kuingia kwenye Mafunzo Haya, kutumia vizuri fursa hii kwa kuwa WAAMINIFU na KUWAJIBIKA kama msingi wa mafanikio, Waache Tamaa waende kwa Hatua.

“ni kaburi peke yake watu waanza kuchimba kuanzia juu kwenda Chini, lakini maisha yananzia Chini kwenda juu” amesisitiza Mhe Mavunde.

Mafunzo haya yanatolewa na Serikali kupitia Fedha za walipata KODI, hivyo wahakikishe wanatumia vizuri fedha zinazotolewa katika mafunzo Haya mana ni fedha za watanzania, Serikali ya Mhe John Pombe Magufuli imedhamiria kuwekeza kwa vijana kwa kuwajengea UWEZO vijana ili waweze kunufaika na maendeleo ya rasilimali zilizopo nchini.

Imetolewa na kitengo cha mawasiliano Serikalini Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
24/08/2017