MFAHAM NG’WANAMALUNDI, MTU WAAJABU.

Mtu huyo aliyewahi kuutingisha utawala wa Wajerumani, alizaliwa katika ukoo wa kawaida akiwa mcheza ngoma mashuhuri, mwaka wa kuzaliwa kwake haufahamiki ila alifariki dunia mwaka 1936, akiwa tayari mtu mzima. Kahama. Kwa Watanzania wenye umri mkubwa waliopata kusoma historia au kusikia hadithi za makabila, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, hawakukosa kusikia habari ya Ng’wanamalundi. Mtu huyo aliyewahi kuutingisha utawala wa Wajerumani, alizaliwa katika ukoo wa kawaida akiwa mcheza ngoma mashuhuri, mwaka wa kuzaliwa kwake haufahamiki ila alifariki dunia mwaka 1936, akiwa tayari mtu mzima. Watu wengi wamekuwa wakimjadili kwa maoni tofauti, wengine wakimsifu kama shujaa huku wengine wakihusisha uwezo wake na nguvu za giza. Katika makala hii usahihi wa historia yake unaelezwa na mjukuu wake wa pili, Kishosha Sitta (80) mkazi wa Kijiji cha Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayesimulia alivyomfahamu babu yake huyo. Sitta anaanza kueleza kuwa jina halisi la babu yake halikuwa Ng’wanamalundi bali lilikuwa Igulu Bugomola, ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Mwakubunga Nera wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Ng’wanamalundi alikuwa mtoto pekee wa kiume na wa mwisho kati ya wanne, kwa baba yake Bugomola na mama yake, Ngolo Igulu. Sitta anasema Igulu (Ng’wanamalundi), alikuwa na tabia ya uzururaji tangu utotoni na mara nyingi haikuwa rahisi kumkuta nyumbani. Alikuwa mashuhuri kutokana na umahiri wake wa kucheza ngoma na mara nyingi alipokuwa akitembea mitaani alifuatwa na kundi kubwa la watoto. “Hali hiyo iliwachukiza wazazi wengi wenye watoto waliokuwa wakiambatana naye, kiasi cha kumchukia hata Ng’wanamalundi mwenyewe, kutokana na watoto wengi hasa waliokuwa wakitoka familia za wafugaji kutoweka na hiki kilikuwa chanzo cha mifugo mingi kupotea baada ya kutelekezwa na watoto hao,” anasema Sitta. Hali ya kuchukiwa kwa Ng’wanamalundi ilienea pale kijijini kiasi cha kuanza kumkebehi, hasa kutokana na umbo lake refu na miguu yake myembamba kuanzia magotini hadi kwenye makanyagio, ikiwa mirefu kuliko kawaida. Sitta anasema hali hiyo ilisababisha kumdhihaki na kumwongezea chuki zaidi kwa wanakijiji wa eneo hilo waliodiriki kumtukana kwa lugha ya Kisukuma; Sitta anasema, Ng’wanamalundi baada ya kumaliza kula chakula kwa Mtemi Chalya aliondoka na wafuasi wake na akapitia kwenye lile pori akachimba dawa zake na kuondoka kwenda kuendelea na maisha yake. “Katika ngoma zake; Ng’wanamalundi alikuwa na tabia ya kuwatahadharisha mashabiki wake kuacha kwenda wakiwa wamejipaka dawa yoyote ile, anasema. Aliwaambia: “Bing’we akwiziza munho wibilaga bugota bosebose ulu kutora akotora henaha,ulo nsabo akupandika heneha.” Kauli hiyo ilikuwa na maana nyie asije mtu amejipaka dawa yoyote hapa kama ni kuoa, ataoa hapahapa kama ni mali atapata hapahapa, hata hivyo kuna wale walipuuza kauli hiyo kwa kuja wamejipaka dawa kwa lengo la kujipima uwezo wa dawa zao. Lakini hawakufanikiwa na badala yake walikufa.