MCHUNGAJI AJIUNGA ACT WAZALENDO

MCHUNGAJI AJIUNGA ACT WAZALENDO

Na John Marwa
darmpya:Updates#Mchungaji wa Kanisa la Kanisa Bethel Grace Church Mission Tanzania la Jijini Arusha,Baltazar Yae leo namejiunga na Chama cha ACT Wazalendo.

Mchungaji huyo alianisha sababu ya kuchukuwa uamuzi ni kutokana na kufurahishwa na siasa za masuala za Chama hiki na kwamba kila akiwasikiliza anaona wanazungumzia mambo yanayomgusa mtanzania moja kwa moja.

“Nimefurahishwa na mkazo wanaoutoa kwenye kilimo na nimeguswa na mapambano yao ya kupigania hali za maisha ya watanzania,” alisema.

Alielezea sababu nyingine kuwa ni pamoja na uelekeo wa sasa wa Chama kwa kutetea bila kuchoka haki za kiraia na demokrasia.

Alisema, amejiunga na Chama hicho akiamini ACT ni jukwaa muafaka kushiriki siasa za Arusha na nchi na kwaba ana imani kupitia Chama hicho atatoa mchango wake kwa Taifa.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*