MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA MHE. STANSLAUS MABULA ATIMIZA AHADI ALIYOITOA.

Mbunge jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula atimiza ahadi yake aliyoitoa tarehe 16 September 2017 Kata ya Mhandu katika Kanisa la Sabato. Mhe Mabula amekabidhi mifuko arobaini ya Cement katika uongozi Wa Kanisa hilo hivi Leo ahadi aliyoitoa alipokuwa na mwendelezo wa ziara kata zote za halmashauri ya jiji la Mwanza kuelezea utekelezaji Wa Ilani ya uchaguzi katika makundi maalum ya kijamii. Mhe Mabula akikabidhi mifuko hiyo amesema “mifuko hii ikawe chachu kwa waaumini na wana Nyamagana kuzidi kuwa wamoja kama ambavyo tumerithi kwa waasis Wa Taifa letu ambao wametulea pasipo kuwa na ubaguzi Wa kitikadi, hivyo basi Wana Nyamagana na watu wote wenye mapenzi mema tujijengee utamaduni wa kushiriki ujenzi wa nyumba za Ibada kwa kadri tulivyo barikiwa na Mungu, kwa kujitolea kwa hali na Mali. Hata kama Serikali yetu ya Tanzania haina dini tukumbuke watanzania wana dini. Kwaniaba ya uongozi Wa Kanisa mchungaji kiongozi amemshukuru Sana’a mhe Mbunge kuwathamini na kuwajari kuungana nao katika Ujenzi Wa Kanisa. Imetolewa na:- Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Nyamagana.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*