MASHABIKI WAVAMIA NYUMBA YA ALEX NG’ONGA BAADA YAKUSHINDWA KUFUNGA GOLI. 


 Polisi nchini Zambia wamewakamata mashabiki watano kwa madai kuwa walivamia nyumba ya mwanasoka watimu ya taifa ya kandanda Alex N’gonga.

Mashabiki hao walishikwa na hasira kuwa Ng’onga alikosa nafasi wazi za kufunga wakati wa mechi muhimu ya kufuzu kwa kombe la dunia ambapo Nigeria iliishinda Zambia bao 1-0
Mambo muhimu kuhusu nchi ambazo tayari zimefuzu Kombe la Dunia 2018
Mashabiki walitoa hasira zao kwa kuvamia nyumba yake iliyo mji wa Kitwe ambao waliitupia mawe, kwa mujibu wa kamishina wa polisi Charity Katanga.
“Tumekamata watu watano kwa makosa ya kuharibu mali na sasa wanazuiliwa na polisi.”
Kushindwa kwa Zambia kuliipokonya fursa ya kufuzu kwa kombe la dunia nchini Urusi ambapo Nigeria walifuzu.