MAREKANI NA URUSI ZAKUBALIANA KUSITISHA MAPIGANO SYRIA.

Rais wa Marekani Donald Trump na  rais Vladimir Putin  wa  Urusi jana  Ijumaa  walikubaliana  mpango  wa  kusitisha  mapigano  katika maeneo  ya  kusini  na  magharibi  mwa  Syria , ikiwa  ni  jaribio  la hivi  karibuni  kabisa  la  kusitisha  umwagikaji  wa  damu  katika  nchi hiyo  iliyoharibiwa  kwa  vita.

Makubaliano  hayo  yataanza  kutekelezwa  mchana  saa  za  Syria siku  ya  Jumapili, wanadiplomasia  wa  ngazi  ya  juu  wa  Urusi  na Marekani  wamesema  wataka  wakitangaza  makubaliano  hayo yaliyofikiwa  na  viongozi  wao  pembezoni  mwa  mkutano  wa  kilele wa  kundi  la  mataifa  yaliyoendelea  na  yanyoinukia  kiuchumi G20 nchini  Ujerumani.

“Ni mafanikio yetu ya  kwanza ,” amesema  waziri  wa  mambo ya kigeni  wa  Marekani Rex Tillerson akizungumzia  ushirikiano  baina ya  Ikulu  ya  Marekani  White House  na  Kremlin.

Shirika  linaloangalia  haki  za  binadamu  nchini  Syria  limesema makubaliano  hayo  ya  kusitisha  mapigano  yalikuwa  yanatarajiwa kujumuisha  miji  ya  Daraa, Sweida  na  Queitra.

Shirika hilo limesema  katika  taarifa  iliyotolewa  juzi Ijumaa  kwamba makubaliano  hayo  yatashuhudia  kuondolewa  kwa  majeshi  ya serikali  ya  Syria  kutoka  katika  mstari  wa  mbele  na  kurejea katika  makambi.

Wakimbizi kurejea nyumbani

Eneo  hilo litatayarishwa  kuwapokea wakimbizi  wa  Syria  kutoka Jordan. Pia  ina  maana  ya  kuruhusu misaada  wa  kiutu  kuwasili katika  eneo  hilo.

Vita  nchini  Syria , ambayo  hivi  sasa  vimo katika  mwaka  wa saba , vimeyaingiza  mataifa  makubwa  duniani  ikiwa  ni  pamoja na  Marekani na Urusi