MAN CITY HII NI HABARI NYINGINE YA KUSISIMUA.

Jana klabu ya Manchester City ikiwa nyumbani imeendeleza ubabe wake katika ligi ya Uingereza msimu baada ya kuibuka na ushindi mnono wa jumla ya mabao 7-2 dhidi ya timu ya Stoke City.

City inayonolewa na Mhispania, Pep Guardiola ilionekana kutakata hiyo jana kwa kuchomoza na ushindi huo mnono bila mshambuliaji wake, Aguero lakini imeweza kufanya vizuri na kuonyesha maajabu katika ligi hiyo ya Uingereza.
Waliyo funga mabao katika mchezo huo kwa upande wa City ni Gabriel Jesus akifunga dakika ya 17’ na 55, Raheem Sterling dakika ya 19, David Silva dakika ya 27, Fernandinho dakika ya 60, Leroy Sane dakika ya 62 na Bernardo Silva dakika ya 79 ya mchezo, wakati kwa upande wa Stoke mabao yakifungwa na Diouf na Kyle Walker.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Manchester City kuwa klabu ya kwanza kufunga jumla ya mabao 29 katika michezo nane ya msimu wa ligi rekodi ambayo iliwekwa na Everton mwaka 1894-95.


Klabu hii ya Manchester City toka kuanza kwa msimu huu wa ligi imecheza michezo nane huku ikitoka sare mmoja na kushinda saba kwa sababu hiyo basi huwafanya wapenzi na mashabiki kutokuwa na wasiwasi kabisa.


Michezo ambayo timu ya Manchester City imecheza mpaka sasa ni pamoja na ule dhidi ya Brighton and Hove Albion ikachomoza na ushindi wa mabao 2-1 tarehe 12 ya mwezi Agosti akiwa ugenini.

Kisha ikatoka sare ya bao 1-1 mbele ya vijana wa Agosti 21 mwaka huu.
Mancheter City ikatoka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Bourne mouth ikiwa ni mchezo wa pili kwake katika ligi ya Uingereza msimu huu.
Kisha vijana hao wa Etihad timu ya City ikaifunga Liverpool kwa jumla ya mabao 5-0 kabla ya kucheza na Watford na kuinyanyasa uwanjani kwa kuifunga mabao 6-1.
Mhispania, Pep Guardiola akawapanga vijana wake sawa akachomoza na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Crystal Palace

 .

City wakaifunga Chelsea bao 1-0 wakiwa ugenini na leo vijana hao wa Guardiola wamchomoza na ushindi huo mnono wa mabao 7-2 dhidi ya Stoke City.