LWANDAMINA AFIKA MAHAKAMANI KUZUNGUMZA NA MANJI

Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amekwenda moja kwa moja hadi katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kuzungumza na bosi wake wa zamani, Yusuf Manji.
Lwandamina alikutana na Manji katika viwanja vya mahakama ya Kisutu akiwa ameongozana na kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa, Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali ‘Mensah’ na Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh.
Manji alikuwa mahakamani hapo kutokana na Kesi inayomkabiri kuhusiana na kutumia madawa ya kulevya imeshindwa kusikilizwa leo katika mahakama ya Kisutu na kusogezwa mbele hadi Septemba 25.
Suala la kushindwa kusikilizwa, limetokana na Manji kuchelewa kufika mahakamani, lakini naye alimueleza hakimu kuwa aliambiwa hakimu yuko katika kikao. Manji anatuhumiwa kutumia madawa ya kulevya, jambo ambalo amekuwa akilikanusha.