KIBARUA CHAOTA NYASI KOCHA WA SUNDERLAND

Meneja wa klabu ya Sunderland muingereza, Simon Grayson ameachishwa kazi baada ya kuihudumia timu hiyo katika michezo 18 pekee toka kuteuliwa kwake.

Grayson ametangazwa kuachishwa kazi dakika 17 tu kupita baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Bolton Wanderersdraw.

Simon Grayson raia wa Uingereza alichukua mikoba ya David Moyes mwezi Juni wakati akitua Sunderland.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimesema

“Sunderland AFC jioni ya leo kwa kushirikiana na meneja Simon Grayson, imeamua kuachana nae na kumpatia shukrani yeye na benchi lake la ufundi kwa jitihada zao kubwa walizofanya katika klabu hii.” Imesema taarifa kutoka Sunderland.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 amefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu toka akabidhiwe nafasi hiyo.

Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Glynn Snodin alishaondoka bila klabu hiyo kutoa maelezo ya nani atarithi nafasi yake wakati ikikabiliwa na mchezo wa derby siku ya Jumapili dhidi ya Middlesbrough.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*