JESHI LA ZIMBABWE LACHUKUA MADARAKA YA KUSIMAMIA NCHI

Mkuu wa Majeshi ya Zimbabwe Jenerali Constantino Chiwenga amesema kupitia kituo cha Taifa cha Television cha Zimbabwe(ZBC) kuwa, wameamua kuingilia kati na kusimamia maswala yote yanayoihusu Zimbabwe kuanzia leo alfajiri.

“Kwanza tunawahakikishia wananchi na taifa kwa ujumla kuwa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Zimbabwe Comrade Robert Gabriel Mugabe na familia yake wako salama na ulinzi wao ni wa uhakika”, alosema General Chiwenga,

‘Tunachokifanya sisi kama jeshi ni kuhakikisha waharifu wote wanaomzunguka Rais wanaofanya uharifu unaosababisha kuteseka kwa nchi na wananchi wake kiuchumi na kijamii wanatiwa nguvuni na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” aliongeza.

Aidha alifafanua kuwa, baada ya kukamilisha jambo hili watarudisha madaraka haraka sana kwa serikali iendelee na majukumu yake kama kawaida kwa mhimili wa mahakama.

Akasema, hizi hatua ambazo jeshi limechukuwa ni kuhakikisha kwamba ninyi kama mhimili huru wa serikali unakuwa huru kufanya kazi zako bila vitisho ama hofu toka Kwenye hili kundi la waharifu kama ambavyo imekuwa siku zote

“Kwa bunge letu, Majukumu yenu ni ya umuhimu mkubwa sana ya amani na utulivu kwenye hii nchi,na ni mategemeo yetu kisiasa tumechukuwa haya madaraka ili kuwapa ninyi nafasi kuhudumia majimbo yao kulingana na majukumu yenu ya kidemokrasia, wananchi wote wa Zimbabwe tunawasisitiza kupunguza mizunguko isiyo ya lazima katika kipindi hiki ” alisema.

Pia aliwaomba wale wote walioajiliwa na wenye biashara kwenye miji kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kwamba ni mategemeo yeo kuwa watafurahia matumizi ya uhuru weo na haki zao kwamba wamerudisha nchi katika mazingira ambayo yanaruhusu uwekezaji,maendeleo na ukuwaji wa nchi ambao wote tuliupigania na raia wetu walijitoa mhanga kwao.

Amevisisitiza kuwakataza wanachama wenu kujihusisha na vitendo vya fujo, na amewaasa vijana kwamba hatma ya nchi iko mikononi mwao na kwamba wasihadaike na pesa chafu, wawe na nidhamu na mbaki watiifu kwa misingi ya taifa lao kubwa.

Kwa upande wa madhehebu ya dini,amewaomba kwenye mikusanyiko yao kuliombea taifa na wahubiri neno la upendo,amani umoja na maendeleo.

Akasema,”kwa watu wetu na kwa dunia nzima tunapenda kuweka wazi kuwa hii hali si hali ya Jeshi kuchukuwa serikali kwa maana ya mapinduzi ya kijeshi.

Jeshi la Zimbabwe linachokifanya ni kusimamia na kushikiria mmomonyoko wa kisiasa, kijamii na kiuchumi ambao nchi yetu inapitia kwa kipindi hiki.

Mwisho:taarifa hii imetafsiriwa na mtandao wa darmpya.com kutoka kwenye taarifa ya Mkuu wa Majeshi ya Zimbabwe iliyotolewa leo alfajiri 15/11/2017 alipokuwa anazungumza.
Fuatilia kwa makini Kwenye blog yetu ya darmpya.com kwa kupata kila kinachotokea

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*