INASHANGAZA SERIKALI KUWEKA MKATABA WA TRILIONI 7 KUJENGA RELI BILA KUSHIRIKISHA SEKTA NYINGINE- MH.ZITTO

Mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha ACT Wazalendo, Mh.Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma, amesema kuwa, ni jambo la kushangaza kuona Serikali ikasaini mkataba wa shilingi Trilioni 7 kujenga Reli bila kuweka vifungu vya kufungamanisha na sekta nyingine nchini.

Mh.Zitto akahoji kuwa, inawezekanaje kweli hata misumari ( screws) nchi hii haiwezi kutengeneza mpaka iagizwe kutoka Uturuki na kwamba yani hata kampuni ya kuchimba kokoto itoke Uturuki,”? alihoji.

Akiendelea kuonyesha kushangazwa na jambo hilo alisema kuwa, mpaka serikali itegemee malighafi hizo kutoka nje hivi viwanda vya chuma nchini CTI, TPSF vinafanya kazi gani sasa.

“Nielezeni hili, hamuwezi kuzalisha kitu chochote kulisha ujenzi wa Reli ya Kati ya SGR katika BOQ ya Mradi wa SGR, hamna muwezalo? Serikali iliwapa BOQ mkashindwa?” alihiji Mbunge huyo.

Akasema, ata ukiwauliza watu wa Wizara hawana majibu, wanasema Mkataba ali alifanya makubaliano Rais mwenyewe.

Aidha aliendelea kusema kuwa, inawezekanaje kuamini hili na kwamba hawezi kumuuliza rais na kwamba wao kazi yao ni kukosoa tu.

“Amekasirika, Siwezi kumwuliza mtu aliyekasirika, tena Amiri Jeshi Mkuu” alisema.

Wakati wa Mdororo wa Uchumi Asia mwaka 1997-1998 Waziri Mkuu wa Malaysia Tun Mahathir Mohammed alifanya miradi mikubwa sana ikiwemo kujenga Mji Mpya, barabara kubwa na Jengo la Petronas.

Ili kuingiza fedha kwenye uchumi na kuchochea shughuli nyengine za uchumi na kukuza mahitaji ( aggregate demand). Malaysia ikawa nchi ya kwanza kuibuka kutoka Asian Financial Crisis.

Aliongeza kuwa, sisi watawala wetu wamekwenda madarasa tofauti na kusoma vitabu tofauti vya Uchumi? Unajenga Reli kwa pesa yako ( inavyodaiwa), kwa hiyo unakusanya kodi kutoka kwa watu wako, unanunua US$, unamlipa Mkandarasi. Mkandarasi ananunua kila kitu kutoka nchini kwao Uturuki, mataruma ya Reli, Chuma, Screws na Misumari na hata mchimba kokoto Mturuki.

“Kwenye uchumi hii inaitwa leakages. Uchumi wetu unahitaji more inflows, unajengaje Reli kwa kutumia Chuma kutoka nje wakati una hazina ya chuma Ludewa?, unamwaga TZS 7 Trilioni bila kuhakikisha offsetting? Natamani kuiona hiyo BOQ ya Reli ya Kati”, akasema Mh.Zitto.

Alisema, suala hili linanisumbua sana, ni vigunu kuamini kuwa watawala waliokwenda shule na wenye uzoefu Serikalini hawakuona faida kubwa ya offsets na kwamba Baraza la Mawaziri limejaa wasomi wenye PHDs, inashangaza kuona kama ni kweli wameshindwa kuona hili.

Alimaliza kusema kuwa, fedha zetu wenyewe tunatengeneza ajira nje ya nchi huku sisi tukiwa vibarua tu na wagonga reli, Trilioni 7 zingechochea sana uchumi.akasema, kutokana na hili ni vyema watetezi wa Serikali, mnaojua kuitafsiri Serikali, lifanyieni kazi suala hili. nisaidieni.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*