IGP SIRO ATEMBELEA KIJIJI CHA MANGWI KIBITI

Siku moja baada ya kuripotiwa mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, IGP Simon Sirro ametembelea kijijini hapo kutoa pole kwa wafiwa.

Aidha, IGP Sirro amewataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo akiwataka kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.
IGP Simon Sirro akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mangwi, Kata ya Mchukwi alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji.

Source:darmpya.com