HIZI HAPA KAULI 20 ZA POLEPOLE KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 18 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA.

Tarehe 13 October katika kipindi cha kipima joto ambacho hurushwa na kituo cha televisheni cha ITV katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi Ndg Humphrey Polepole alipata nafasi ya kuongea, na hapa tumekuwekea kauli zake 20 katika kuelekea maadhimisho ya miaka 18 ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“Yule anayedhibiti fedha ndio anayedhibiti siasa, Serikali ya awamu ya tano imejipambanua kuleta uhuru wa kiuchumi”

“Katika muktadha wa sasa tangu Mwalimu ametutoka aliacha hotuba ya ubashiri wa kuibuka kwa  viongozi   watakaokua na uchungu kwa  Rasilimali zetu tunaona sasa kwa Ndg. John Pombe Joseph Magufuli.”

“Umadhubuti wa Taifa letu umejengwa na tunu ya Umoja, kama watu wachache kwa maslahi yao wanachochea chuki na kuvuruga tunu hii ya umoja ni lazima tuwakemee”

“Mwalimu aliamini uchumi imara ni uliojengwa na miundombinu imara na yenye bei nafuu mfano ujenzi wa Reli ya kisasa hapa kwetu”
“Sasa tunakwenda kutimiza ndoto ambayo haikutimizwa na Mwalimu nayo ni ujenzi wa Stiglres george”

“Kujitegemea kiuchumi ni moja kati ya hili tulilolianza nalo sasa la kudhibiti Rasiliamali zetu na hili linafanywa na kiongozi wa awamu ya tano Ndg. John Joseph Pombe Magufuli”.

“Kwa mara ya kwanza unafanyika mnada wa kwanza Mererani wa kununua Tanzanite katika pahala ambapo Tanzanite inachimbwa haijapata kutokea katika historia ya Taifa letu”

“Leo hii tunayoa Elimu bure kutoka kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne mwalimu Nyerere alianza na UPE darasa la kwanza mpaka la saba”

“Ushahidi unaonesha tangu tutamke hili la Elimu bure shule iliyokuwa inachukua watoto 300  sasa inapata watoto 600 tafsri yake watoto wa maskini wamepata uwezo wa kupata elimu”
“Huu ni mwaka 2017 uchumi wa Tanzania nidhamu yake imeimarishwa sana tafsri yake pesa inayopatikani kwenye uchumi huu ulioimarika ndio hiyo inayoenda kutibia wazee wetu bure”

“Mwalimu alitamani kuona utimilifu wa kufikia ustawi wa maisha ya watanzania na alifanya kwa nafasi yake”
“Uongozi wa awamu ya tano sasa umejikita na kushughulika na shida za watu wake”
“Kuondoa Umasikini maana yake ni kuondoa tozo zote zenye maudhi kwa mkulima  wa chini na kupeleka pembejeo na ruzuku kwa wakati na pasina kuweka mizengwe”

 “Na mtu yeyote anayefanya mizengwe na pembejeo za watu wetu ni wa kushughulika nae kwa ukali zaidi”

“Kuondoa umasikini maana yake ni Lindi, Mtwara na Pwani tunapeleka viua wadudu bure kwa kila mkulima anayelima Korosho”

“Kuondoa umaskini tunamaanisha kuweka kilimo cha mkataba tumuwezeshe mkulima tumpe pembejeo, sumu ya kuuwa wadudu halafu alime avune kisha auze mazao yake”
“Tunaposema tunakamata wezi walioiba rasilimali zetu ni lazima tuwe wamoja”
“Tunazungumzia Maleria,  hapo kibaha kipo kiwanda ambacho ni kimoja tu Afrika kinatengeneza dawa  ambayo ni salama kwa matumizi ya binadamu itakayomaliza mbu wote na viluwiluwi vya maleria”

“Tulirithi dola ya Tanganyika na dola ya kule Zanzibar lakini tumeunda wenyewe Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania”

“Kama wapo watu ambao wameona kutafuta umaarufu wa bei nafuu kwa kupalilia mambo yanayodhoofisha umoja wetu tunakila sababu ya kuwakemea na kuwakataa”